Thursday, June 18, 2015

MCHA KUIKOSA KAGAME CUP

Posted By: kj - 6:23 PM

Share

& Comment

Mshambuliaji wa Azam FC, Mcha Hamis amewekwa bandeji ngumu P.O.P kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kupata majeruhi kwenye goti lake la mguu wakushoto, hivyo amepewa mwezi mmoja kuwa nje ya Uwanja na atakosa mashindano ya Kombe la Kagame.

Kwa mujibu wa daktari wa Azam, Mbaruku Mlinga alisema, ili Mcha apone kabisa na kurudi uwanjani, atakaa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

"Alivunjika kidogo kwenye goti ndiyo maana tukamwekea P.O.P ili awe sawa. Atakaa na bandeji hiyo kwa muda wa wiki mbili na tangu alipowekwa hadi leo, ameshamaliza wiki moja hivyo Alhamisi ijayo atatolewa,"alisema Mbarouk.

"Baada ya hapo, ataanza mazoezi mepesi kama wiki mbili ndiyo atarudi uwanjani akiwa vizuri kabisa na kwa maana hiyo, upo uwezekano  akakosa mashindano ya Kagame."

Mbaruku amesema, wachezaji wengine ambao wana program maalum ni  beki wa kushoto, Waziri Salum aliumia unyayo Congo, beki wa kati, Abdalah Kheri alichanika nyama paja na program anayofanya ni kuweka sawa, jeraha lisiweke kovu.

Wengine ni Joseph Kimwaga aliyefanyiwa upasuaji Afrika Kusini na programu yake ni kumfny apone kabisa na Farid Mussa alikuwa anasumbuliw na nyama za paja amepona kabisa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.