Tuesday, September 27, 2011

MITIHANI MEMA HIMID MAO

Posted By: kj - 6:56 AM

Share

& Comment

Kiungo chipukizi wa Azam FC, Himid Mao ni miongoni mwa watahiniwa wa mwaka huu, ambapo wanatarajiwa kuanza mitihani yao hapo october 3.

Viongozi wa Azam Fans Club unamtakia mitahini mema Himid Mao pamoja na watahiniwa wengine na unamuombea dua afanye vyema katika mitihani hiyo ya kidato cha nne.

Mao ni miongoni mwa wachezaji walio ibuka kupitia Copa coca cola na kupata nafasi ya kujiunga na Azam Academy na kupandishwa katika kikosi cha Azam FC.

Himid Mao alikiongoza kikosi cha Azam Academy pale ilipotwaa Uhai Cup kwa mara ya kwanza katika msimu wa 2008/2009 na msimu ulio fuata alianza kupewa nafasi katika kikosi cha Azam FC.

Mao amekuwa kapteni katika timu za vijana za taifa kuanzia ile ya chini ya miaka 17 mpaka chini ya miaka 20.

Mitihani mema Himid Mao, twakungoja kwenye pitch baada ya kumaliza mitihani yako.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.