Sunday, November 13, 2011

Azam yakataa ofa ya Simba

Posted By: kj - 3:19 PM

Share

& Comment

UONGOZI wa klabu ya Azam FC umetakaa ofa ya klabu ya Simba kutaka wabadilishane mchezaji mmoja kwa wawili.

Simba iliwasilisha maombi kwa Azam ikitaka wabadilishane Emmanuel Okwi na wao wamrudishe kundini kiungo wao wa zamani, Ramadhan Chombo 'Redondo' pamoja na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche.

Msemaji wa Azam FC, Jafar Iddi alisema kuwa uongozi wa Simba uliwasilisha barua kwao ukiomba kufanyika kwa makubaliano baina ya wachezaji hao lakini baada ya uongozi wa klabu yake kutafakari kwa kina uliona hakukuwa na umuhimu wowote wa kufanya hivyo kwa sasa.

"Kuna jambo moja hapa, Simba walituletea barua hapa wakiomba watupe Okwi na sisi tuwape Kipre Tchetche na Redondo lakini tumekataa kwa sababu tayari tumeachana na wachezaji wawili kutoka Ghana (Wahab Yahya na Nafiu Awudu) na kuwaachia hawa kutaua nguvu ya Azam," alisema.

Alisema kuwa klabu yake kwa sasa inatafuta wachezaji kwa ajili ya kuongeza nguvu kikosi chao na si kuwatoa na kama kuna timu inamwitaji mchezaji wao hawatakuwa tayari kumuuza.

"Dirisha dogo si wakati wa kuuza wachezaji ni wakati wa kuimarisha kikosi, hivyo basi si hawa tu kama kuna timu nyingine pia zinawataka wachezaji wetu haitawezekana," alisema.


Mwananchi

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.