Thursday, January 12, 2012
Azam watwaa taji la kwanza
Posted By: kj - 10:53 PMKikosi kazi cha wazee wa gonga kama Azam FC wamefanikiwa kutwa taji la kwanza baada ya kuichapa goli 3-1 timu ngumu ya Jamhuri ya Pemba yenye maskani yake katika vitongoji vya Wete Pemba.
Katika mchezo wa fainali uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Amani uliopo katika visiwa vya Karafuu ambavyo vinahazimisha miaka 48 ya Mapinduzi, Jamhuri walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Iddi Ramadhani katika dakika ya 17.
Goli hilo lilisawazishwa dakika 43 kupitia Kwa mfungaji bora wa Azam FC, John Raphael Bocco na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya goli 1-1.
Jamhuri kama kawaida walitumia mashambulizi ya kushtukiza huku wakijaribu kutoipa mwanya Azam FC kupata goli la ushindi. Na mnamo dakika ya 59 John Bocco ambaye ana rikodi nzuri katika mikwaju ya penati, alipaisha penati na hivyo kuchelewesha sherehe ya Azam.
Kwa kuashilia uzito wa ngoma ya Azam ambapo huwa ngumu kwa timu kuhimili vishindo vyake kwa dakika zote 90, Jamhuri walijikuta wanaruhusu goli la pili lililo fungwa na John Bocco katika dakika ya 88 kabla ya mtokea bench, kijana anaetarajiwa kwenda Marekani kama dili litakamilika Mrisho Khalfan Ngassa kuhitimisha kwa kufunga goli la 3 katika dakika za lalasalama.
Katika historia ya Azam FC kombe la Mapinduzi ndilo kombe lao la kwanza wakati Azam Academy wakiwa na taji la Uhai Cup.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment