NIMEIPENDA MWENYEWE

NIMEIPENDA MWENYEWE

Sunday, December 23, 2012

ACADEMY KUJARIBU KUFUTA MAKOSA YA MWAKA JANA

Posted By: kj - 8:03 AM

Fainali za tano za Uhai Cup zitapigwa leo kwenye uwanja wa karume ambapo zitaikutanisha Azam Academy ambayo itakuwa ikicheza fainali yake ya nne (kati ya tano) na Coastal Union ya Tanga.

Azam Academy inayoundwa na wachezaji wengi wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao wengi wao wanachezea timu ya Taifa ya Serengeti Boys itajiaribu kulitwaa kombe ambalo msimu uliopita ililipoteza kwa Simba SC katika hatua ya penati baada mchezo kuisha dakika 90 kwa matokeo ya sare ya 0-0
 

Pamoja na fainali hizi kuingia mwaka wa tano lakini bado inaonekana wadau hawajaelewa dhana ya mashindano haya kwani tumeshuhudia timu nyingi zikileta vijeba tena baadhi ya wachezaji hao vijeba ni wale ambao walishachezea baadhi ya timu Kama Azam Academy na kuachwa baada ya kuvuka umri.
 

Tatizo hili linapoteza maana ya mashindano na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote

AZAM WAFUNGA MWAKA KWA KUTWAA KOMBE DRC

Posted By: kj - 7:56 AM
Azam fc wamefunga mwaka wa 2012 kama walivyo uwanza mwaka huo kwa kutwaa kombe Charity nchini DR Congo kama walivyo fanya mwanzoni mwa mwaka huu wa 2012 kwa kutwaa kombe la Mapinduzi katika visiwa vya karatuu Zanzibar.

Azam fc jana ilicheza mchezo wa fainali jijini Kinshasa, DR Congo dhidi ya mabingwa wa jimbo hilo la Kinsasha, Dragon na kuibuka na ushindi wa penati 4-2 baada ya kutoka sare ya goli 1-1.

Azam FC ilishiriki michuano hiyo kama timu mwalikwa na kuchukulia mashindano hayo katika maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara na kombe la shirikisho.

Azam FC imeshiriki michuano hiyo bila ya nyota wake waliopo timu ya Taifa ya Tanzania  'Taifa Stars'.
Azam FC jioni hii imetwaa kombe la Congo Charity Cup baada ya kuifunga Dragons kwa penati 4-2 kufuatia sare ya 1-1. Golikipa Mwadini Ally alidaka penati mbili. Hongera Azam FC, Hongera Taifa Stars

Saturday, December 22, 2012

MSUNI ANGOJA ZAWADI YA UBINGWA TOKA AZAM

Posted By: kj - 7:34 AM
Bogger wa Azam Fans Club na mmiliki wa Aboodmsuni Network 'AN' Abdallah H.I Sulayman 'Msuni' jana alifinga ndoa na Bashira mjini Morogoro wakati vikosi vya Azam Academy na Azam FC zikikata tiketi ya kutinga fainali karika michuano inayoshiriki.

Academy waliwafunga Mtibwa sugar kwa mikwahu ya penati 4-3 baada ya kumaliza mchezo wakiwa sare ya goli 1-1 katika nusu fainali ya kwanza ya Uhai Cup iliyochezwa asubuhi kabla ya kaka zao kushinda kw penati 5-4, baada ya kutoka sare ya goli 2-2.

Fainali zote zitachezwa kesho jumaplili december 23, wakati Academy wakicheza na Coastal Union katika uwamja wa Karume jijini Dar es salaam wakati kaka zao watakuwa DRC.


KUTOKA KWA BIN ZUBEIRY
Kipa Mwadini Ally kulia akimpongeza Nahodha wake, Jabir Aziz baada ya kufunga penalti ya mwisho

Na Mahmoud Zubeiry, Kinshasa
AZAM FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Hisani, baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Nahodha Jabir Aziz Stima ndiye aliyekwenda kupiga penalti ya mwisho, Shark wakitoka kupoteza, kufuatia mpira kugonga mwamba. Aiziz aliwainua vitini wachezaji wenzake na makocha wake pamoja na viongozi wa wachache wa timu hiyo waliopo hapa kwa kupiga penalti maridadi iliyotinga nyavuni.
Azam sasa, itamenyana na mshindi wa mechi inayoendelea hivi sasa kati ya Dragons na FC MK Jumapili katika fainali.
Azam iliuanza mchezo huo vizuri na ikicheza kwa maelewano makubwa sambamba na kushambulia kwa kasi kutokea pembeni, kulia Kipre Herman Tchetche na kushoto Seif Abdallah.
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza la Shark liliwapa bao la kuongoza dakika ya 16, lililofungwa na Ngulubi Kilua, baada ya mabeki wa Azam kudhani ameotea.
Iliwachukua dakika 10 tu Azam kusawazisha bao hilo, mfungaji akiwa Gaudence Exavery Mwaikimba aliyeunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya nyota wa mchezo wa leo, Kipere Herman Tcheche kutoka wingi ya kulia.
Baada ya bao hilo, Azam iliendelea kuwashambulia Shark na dakika ya 37, Kipre Tchetche aliifungia timu hiyo bao la pili, kufuatia kazi nzuri ya Mwaikimba. Mwaikimba alipokea mpira mrefu, akatuliza na kumtangulizia kwa mbele mfungaji, ambaye hakufanya makosa, alimchambua kipa wa timu inayomilikiwa na mdogo wa rais wa DRC, Joseph Kabila.       
Hadi mapumziko, Azam ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1 na kipindi cha pili Shark waliingia kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha kwa penalti dakika ya 47, iliyotiwa nyavuni na Bukasa Kalambai, ambaye yeye mwenyewe alijiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kuzongwa na beki David Mwantika.
Baada ya dakika 90 kutimu timu hizo zikiwa zimefungana 2-2, sheria ya matuta ilichukua mkondo wake na wachezaji wote watano wa Azam waliopewa dhamana hiyo leo na kocha Muingereza Stewart Hall, walitimiza wajibu wao vizuri.
Kipre Tchetche alifunga ya kwanza, Mwaikimba ya pili, Jaockins Atudo ya tatu, Himid Mao ya nne na Stima akapiga ya ushindi.
Stewart alisema amefurahishwa na matokeo ya mchezo wa leo na sasa ana matumaini ya timu yake kurejea na Kombe hilo Dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Hajji Nuhu, Joackins Atudo, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou, Seif Abdallah/Uhuru Suleiman dk 77, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno na Gaudence Mwaikimba. 

Wednesday, December 19, 2012

ACADEMY WATINGA NUSU, KUCHEZA NA MTIBWA IJUMAA

Posted By: kj - 4:47 PM
Azam academy wametinga hatua ya nusu fainali ya uhai cup (koabe la vikosi B vya VPL) baada ya kuwafunga goli 1:0 JKT Ruvu katika mchezo wa robo faieali ulichezwa mapema leo.

Madogo hao wa azam sasa watawakabhli Mtibwa sugar siku ya ijumaa

Monday, December 17, 2012

ACADEMY MAMBO SAFG UHAI

Posted By: kj - 8:02 AM
Azam Academy jana imetinga robo fainali za michuano ya Uhai cup baada ya kuifunga Simba Kids 3-2 katika mchezo wa kuvutia uliochezwa kwenye uwanja wa Karume, Magoli ya Azam Academy yalifungwa na Joseph Kimwaga na Adam Omary

ACADEMY MAMBO SAFG UHAI

Posted By: kj - 8:02 AM
Azam Academy jana imetinga robo fainali za michuano ya Uhai cup baada ya kuifunga Simba Kids 3-2 katika mchezo wa kuvutia uliochezwa kwenye uwanja wa Karume, Magoli ya Azam Academy yalifungwa na Joseph Kimwaga na Adam Omary

Monday, December 10, 2012

AZAM; SOMBA WA:ITANGULIA KUVUNJA MKATABA

Posted By: kj - 9:29 AM


Na Mahmoud Zubeiry
 
KLABU ya Azam FC imesema kwamba, Simba SC ilikiuka mkataba wao wa kuwauzia kwa mkopo mchezaji Mrisho Ngassa kwa kitendo cha kumsainisha mkataba nyota huyo na kumpa gari aina ya Verosa na Sh. Milioni 18.
 
Taarifa ya Azam kwa BIN ZUBEIRY, imesema kwamba, wanashangaa Simba kulalamikia Azam kumuuza El Merreikh ya Sudan bila ya kufikia nao makubaliano, wakati wao walianza kukiuka mkataba. 
 
“Kwanza tunapenda umma uelewe kwamba, sisi tuliwashirikisha Simba mapema tu katika mpango huu, lakini wao wakataka fedha nyingi, ambazo Merreikh hawakuwa tayari kutoa, na sisi kwa kuzingatia maslahi ya mchezaji na taifa, tukaamua kutumia haki yetu, akiwa mchezaji wetu kwa kuamua kumuuza,”imesema taarifa ya Azam.
 
Azam imeliandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juzi ikiwaomba wamruhusu Ngasa kwenda Sudan kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya katika harakati zake za kujiunga na El Merreikh ya nchini humo.
 
Azam FC imesema kwamba, katika barua waliyowapelekea TFF, nakala wamewapelekea pia na Simba SC, ambako mchezaji huyo alikuwa anacheza kwa mkopo.
 
“Msukumo uliotufanya tuandike barua hii ni kwa kutambua kuwa hii ni nafasi muhimu kwa Ngassa na taifa, kwani anakwenda kucheza kwenye timu yenye uwezo na miundombinu mikubwa barani Afrika, na inayoshiriki ligi ya mabingwa Afrika karibu kila msimu, kitu ambacho kitamuongezea Ngassa kiwango na kuwa na msaada kwa tafa,”ilisema taarifa ya Azam.
 
Aidha, Azam wamesema pia wanapenda kuweka wazi thamani ya usajili na mshahara ambao Ngassa. Wamesema Ngassa atakuwa anapewa na El Merreikh mshahara wa dola za Kimarekani 4,000, kiasi cha Sh. Milioni 6 za Tanzania kwa mwezi, ambazo kwa miaka miwili ni takribani Sh. Milioni 144 Milioni.
Wamesema mchezaji huyo amepewa fedha za kusaini dola za KImarekani 50,000, kiasi cha Sh. Milioni 80.
 
“Kwa hiyo Ngassa ataweka kibindoni zaidi ya Shilingi Milioni 230 kwa miezi 24, hizi ni fedha nyingi kwa mchezaji wa kitanzania na kwa maendeleo ya mchezaji na familia yake na yatawapa msukumo vijana wengi wenye kipaji kama Ngassa kufanya bidii kwenye soka na kuliletea maendeleo taifa,”ilisema taarifa ya Azam.
 
Azam FC imeomba TFF imruhusu Ngassa kwenda Sudan akitokea Uganda kwenda kukamilisha vipimo vya Afya na usajili na Azam FC ipo tayari kukaa na Simba na kuzungumza juu ya uhamisho huu kwa usimamizi wa TFF.
 
"Hapa ieleweke kuwa ingawa Azam FC inajua haki zake kisheria, lakini pia imeamua kupunguza msimamo wake kukubali mazungumzo kwa kuangalia zaidi athari ambazo mchezaji anaweza kupata kimaslahi na kimaendeleo ya uchezaji wake na mpira wa Tanzania kwa ujumla kutokana na mgogoro huu,”iliongeza taarifa hiyo.
 
Lakini Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema klabu yake haiko tayari kufanya mazungumzo na Azam FC juu ya suala hilo.
 
Kaburu amesema, klabu yake iliingia mkataba na Azam FC kwa kununua haki zote za huduma za Ngassa kwa mwaka mmoja, hadi Mei 21 mwakani, ikilipa Sh. Milioni 25 kama ada ya kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja pamoja na kumlipa mchezaji haki zake zote stahiki za kimkataba ikiwemo mshahara wake.
 
Kaburu amesema Azam bila ya kuzingatia mkataba iliousaini na Simba SC, na matakwa ya FIFA yanayohusu mkopo, iliamua kutangaza kumuuza Ngassa bila ya kuihusisha Simba wakati ikijua kuwa ilikuwa na Mkataba na Simba SC ambayo ameishaichezea katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.
“Kitendo cha Azam FC kuongea na Klabu ya El Merreikh FC na kuweka makubaliano ya mauzo ya mchezaji na kumtangaza kuwa kimemuuza mchezaji Ngassa bila ya kuihusisha Simba SC, na baadaye kuiandikia klabu ya Simba kuwa kimeamua kumrudisha mchezaji Ngassa Azam, wakati ikijua kuwa ina mkataba na Simba SC ni uvunjifu mkubwa wa taratibu na umeleta athari kubwa kwenye klabu yetu,”alisema Kaburu na kuongeza;
 
“Tayari Simba SC ilikwishatuma malalamiko TFF na kupeleka pingamizi lake juu ya sulala hili kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, ambapo imeamuliwa kuwa suala hili liende kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi ya Wachezaji likapatiwe ufumbuzi,”alisema.
 
Amesema Simba imekuwa ni klabu yenye kuangalia zaidi maslahi ya wachezaji na haina kipingamizi kwa kuwaruhusu wachezaji wake kutoka pindi wanapopata timu nje ya nchi kama utaratibu unafuatwa.
 
Kaburu amesema Simba SC ilikuwa tayari kukaa mezani na Azam kwa mazungumzo, lakini kwa kuwa Azam haipo tayari kutambua haki za Simba SC na imekuwa ikilitekeleza suala hili kiholela, hivyo haioni sababu za kuzungumza na Azam FC na kuliacha suala hili liende kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi ya Wachezaji kama TFF ilivyoagiza.


Source; BIN ZUBEIRY

Wednesday, December 5, 2012

AZAM KUELEKEA KIONSHASA

Posted By: kj - 10:06 AM
 
Azam FC inatarajia kuelekea Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 13-23 mwezi huu kushiriki mashindano ya Ngao ya Jamii (Charity Cup)

Mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DCMP na AS Vita Club timu kutoka nje ya kongo kama Azam FC, Tusker FC, Gombe United ya Nigeria na Diable Noirs na Congo Brazavile yatatumika na Azam FC kama maanadalizi ya Confederations Cup
Azam FC inahitaji maandalizi na mechi nyingi za kirafiki nje ya Tanzania ili kupata uzoefu kabla ya kushiriki Confederations Cup. Kwa maana hiyo hii ni nafasi muhimu sana kwa Azam FC

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.