Friday, February 8, 2013

AZAM NA MTIBWA KUKWAANA JUMAPILI

Posted By: azam fans - 2:17 PM

Share

& Comment

Mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati ya Azam fc na Mtibwa sugar uliokuwa uchezwe kesho jumamosi katika uwanja wa Manungu complex sasa utachezwa siku ya jumapili keshokutwa katika uwanja huo uliozungukwa na mashamba wa miwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa ndani ya ukurasa wa Mtibwa sugar ndani ya facebook mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku toka kuwa jumam6si mpaka shku ya jumapili ya febuary 10.

Azam iliyo katika nafasi ya 2 ikiwa imejikusanyia jumla ya point 30 ndani ya michezo 15 itateremka katika mchezo huo bila ya beki wake wa kushoto Samih Hajji Nuhu.

Mara ya mwisho kwa azam fc kuutembelea uwanja wa manungu walikubali kichapo cha goli 1-0, kikiwa kichapo cha kwanza kwa azam kukipata katika uwanja huo wa manungu mbele ya wamiliki wa uwanja huo Mtibwa sugar.

Mtibwa sugar walilala mbele ya Polisi moro katika mchezo wa mwisho kwa mtibwa kucheza katika uwanja huo wa manungu kabla ya kwenda taifa kutoka sare na yanga.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.