Sunday, May 26, 2013

"HATUNA MPANGO NA KAPOMBE"

Posted By: Unknown - 10:44 PM

Share

& Comment

Wakati Simba na Yanga wakiendelea na usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya vodacom, timu inayo leta changamoto kwa vigogo hao wa soka nchini Azam FC wao bado hawajaanza mawindo wa kusaka nyota watakao ongeza nguvu katika kikosi chao.

Azam FC wamekuwa wanavumishwa kuanza mazungumzo na beki wa Simba Shomari Kapombe sambamba na kipa wa simba Juma Kaseja ambapo tetesi hizo zimezimwa na uongozi wa Azam FC.

Msemaji wa Azam FC Japhari Iddi Maganga amesema kuwa bado hawajapokea ripoti ya kocha mkuu Stewart Hall, na kupelekea kutokuwa katika mawindo ya mchezaji wowote yule anaye vumishwa kusajiliwa na Azam FC.

Maganga alisema kuwa Azam FC bado hawajaanza mazungumzo na mchezaji yoyote kwa ajili ya msimu ujao, na hawafahamu yupi ataachwa mpaka pale watakapo pewa ripoti ya kocha mkuu.

Maganga amesema kuwa Hall bado yuko nchini na awezi kuondoka mpaka awakilishe ripoti yake na viongozi kuanza kufanyia kazi mapendekezo yake, aliyo yatoa kwa viongozi.

Akizungumzia suala la Kapombe Maganga amesema kuwa taarifa hiyo wamekuwa wakizisoma kwenye magazeti, na kuzisikia katika vijiwe mbalimbali vya michezo.


0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.