Tuesday, August 13, 2013

AZAM KUREJEA LEO KUTOKA BONDENI

Posted By: azam fans - 9:12 AM

Share

& Comment

Makamu bingwa wa Tanzania bara na bingwa wa kombe la Mapinduzi Azam fc wanataraji kurejea nchini hii leo wakitoka Afrika kusini 'Bondeni' walipokuwa na kambi ya mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania bara.

Azam fc wakiwa Afrika kusinu kwa takribani wiki moja na nusu wamecheza michezo 4 ya kirafiki ambapo katika michezo hiyo wameshinda mchezo mmoja na kufungwa yote mitatu iliyo salia.

Wachezaji wote wa azam fc wanaotarajiwa kuiwakilisha timu hiyo katika ligi kuu ya vodacom walikuwepo Afrika kusini isipokuwa kiungo wa Kenya Humphrey Mieno na mshambuliaji toka Uganda Brian Umonyi.

Azam fc wanataraji kushuka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam agusti 17 kuwakabili yanga katika mchezo wa ngao ya jamii. Mchezo utakao ashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Azam fc baada ya mchezo huo wa ngao ya jamii, wataelekea mkoani Morogoro kuwakabili wakatamiwa wa Turiani Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom msimu wa 2013/14.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.