Baada ya kufanikiwa kuwa makamu bingwa mara mbili mfululizo, mbio za kusaka ubingwa wa TAnzania Bara zinatarajia kuanza kesho katika kiwanja cha Manungu Complex, pale kikosi kazi cha AZam FC kitakapo kuwa wageni wa Mtibwa sugar.
Azam FC wameenda leo katika mashamba ya miwa ya Turiani Mkoani Morogoro na kikosi kamili teyari kwa mchezo huo wa ufunguzi wa ligi kuu ya vodacom, ambapo Azamn FC wataendelea kukosa huduma ya kiuongo toka Kenya Humphrey Mieno na mshambuliaji toka Uganda Brian Umonyi walio kuwa majeruhi.
Katika mchezo wa mwisho wa Azam FC katika uwanja wa Manungu walitoka na ushindi wa magoli 4-1 ukishuhudia urejeo mwema wa mshambuliaji Kipre Tchetche.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment