Wednesday, January 29, 2014

TCHECHE AIWEKA AZAM KATIKA UONGOZI WA LIGI

Posted By: kj - 10:33 PM

Share

& Comment


Goli pekee la mshambuliaji kutoka Ivory coast Kipre Herman Tcheche limeiwezesha Azam Fc kukaa kileleni mwa ligi baada ya kuwachapa Rhino Ranger ya Tabora goli 1-0 huku Yanga wakienda sare ya bila kufungana.

Azam FC wamefikisha pointi 33 wakiwa katika uongozi wa ligi wakifuatiwa na Yanga wenye point 32 wakiwa wote wameshuka uwanjani mara 15.

Azam FC leo walikuwa katika uwanja wake waq Azam complexs uliopo Chamanzi kuwakaribisha wajeda wa Rhino Rangers na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Tcheche akitafuta namna ya kumtoka mlinzi wa Rhino

Bao pekee la Azam limefungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 31 kwa shuti kali baada ya kuukuta mpira uliozuiwa na mabeki wa Rhino, kufuatia shuti la ndugu yake kutoka nchi moja, Ismael Kone.

Goli hilo limemfanya mfungaji bora wa msimu uliopita Tcheche amfikie mshambuliaji wa Simba Hamisi Tabwe aliyefunga magoli 10  ambayo Tcheche ameyafikisha hi leo

Azam FC hii leo waliwakilishwa na Mwadini Ally, Maliki Ndeule, Erasto Nyoni, Aggrey Morrice, Said Moradi, Kipre Bolou, Himid Mao, Salum Aboubakari,Kone, Kipre Tcheche na Joseph Kimwaga

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.