Goli pekee la mshambuliaji toka Ivorycoast Kipre Herman Tcheche limeielekea Azaqm Fc kuanza kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0 katika michuano ya kombe la shirikisho barani Africa, kufuatia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya Ferroviario ya Msumbiji.
Azam Fc wakicheza kwa mara ya kwanza michuano ya CAF katika uwanja wao wa Azam complexs uliopo Chamanzi nnje kidogo ya jiji la Dar es salaam iliwabidi wangoje mpaka dakiak ya 41 ndipo mshambuliaji aliye katika kiwango bora Kipre Herman Tcheche kuiandikia Azam FC goli pekee la ushindi.
Mchezo wa marejeano unataraji kuchezwa mwishoni mwa juma hili kati ya februari 14,15 au 16. Ambapo Azam FC inataraji kuelekea Msumbiji kwa ajili ya mchezxo wa marejeano siku ya jumatano.
Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo kiliundwa na: Mwadini Ally, Malik Ndeule, Erasto Nyoni, Aggrey Morice, aid Moradi, Kipre Bolue, Himid Mao, SalumAboubakari, Briany Umonyi, Kipre Tcheche na Khamisi Mcha.
Sunday, February 9, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment