Saturday, February 8, 2014

BOCCO HUENDA AKAREJEA KESHO

Posted By: Unknown - 4:04 PM

Share

& Comment

Mfungaji bora wa wakati wote wa Azam FC John Raphael Bocco huenda jumapili akarejea uwanjani wakati Azam FC wakicheza mchezo wao wa kwanza wa kombe la shirikisho bara Afrika.

Japhari Iddi Maganga alisema kikosi cha Azam FC kitakuwa na nguvu kubwa hapo kesho baada ya mshambuliaji wake, John Bocco kuruhusiwa kucheza mechi hiyo na nyingine zinazokuja baada ya kubainika kuwa amepona.

Juzi, Idd alisema Bocco hatakuwepo kwenye mechi hiyo kwani alikuwa akisumbuliwa na majeraha, na wakati anaeleza toka apate majeraha alikuwa ameshapumzika wiki mmoja na alitakiwa wiki mbili.

“Bocco atacheza katika mechi ya Jumapili na nyingine za Ligi Kuu, kwa sababu tayari imethibitishwa kuwa amepona majeraha yaliyokuwa yakimkabili, ujio wake utatusaidia kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji,” alisema msemaji huyo.

Alisema mchezaji mwingine ambaye amebainika kuwa na majeraha ni Joseph Kimwaga ambaye alipandishwa kutoka timu ya vijana msimu huu na kuonekana kufanya vizuri zaidi kwenye kikosi hicho.

Alitaja pia viingilio kwenye mechi hiyo kuwa ni Sh 2,000, 5,000 na 7,000 na kuongeza kwamba wameweka viingilio vidogo ili kuwapa fursa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia Azam ishinde mchezo huo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.