Mbali na hilo, pia amemtupia lawama mwamuzi wa mchezo huo, Hashim Abdallah, naye alikuwa chanzo katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa dimba la Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ongala alisema, kipindi cha kwanza vijana wake walionekana kutawaliwa na hofu kubwa ya mchezo na kujikuta wakishindwa kupata bao la mapema licha ya kupata nafasi nyingi.
Alisema wanamshukuru Mungu kwa kuvuna pointi moja katika mchezo huo kuliko kupoteza, kwani matarajio yao makubwa ilikuwa ni pointi tatu katika mchezo huo.
“Leo kusema kweli tulijipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi, ila ndio mpira, lakini wachezaji wangu walikuwa na hofu kubwa hasa kipindi cha kwanza ila cha pili walijitahidi na kuondoa hofu hiyo,” alisema na kuongeza kuwa, katika mchezo huo hawakumtumia kinda mahiri, Joseph Kimwaga, kutokana na kuwa majeruhi.
Aidha, Ongala alimtupia lawama mwamuzi Hashim Abdallah kwa kutokuwa na maamuzi sahihi, hasa baada ya kukataa bao lao lililofungwa na Kipre Tichtche kwa madai ya beki wa Yanga, Juma Abdul kuchezewa rafu.
Aliwataka waamuzi kuchezesha kwa usawa na haki, ili mshindi apatikane kwa uhalali na si kubebwa, huku akidai sasa nguvu zao wanazielekeza katika mchezo wa Jumapili dhidi ya JKT Oljoro.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment