Azam FC kama ilivyokuwa katika misimu miwili iliyo pita mpaka kufikia michezo ya 19 walikuwa bado wamo katika mbio za Ubingwa na kwa mara ya pili mfululizo mbio za ubingwa zinabakia kwa Yanga na Azam FC.
Yanga jumamosi wao watakuwa wanacheza mchezo wao wa 18 wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri kabla ya kuikabili Azam FC siku ya jumatano machi 19 mwaka huu.
Azam FC ambayo mpaka sasa haija poteza mchezo wowote ule ili wa twae ubingwa kwa mara ya kwanza inabidi kupata matokeo katika mechi 8 zilizo salia, amapo moja wapo ni dhidi ya Yanga iliyobakisha michezo 9 wakiwa na point 39 point moja nyuma ya Azam FC yenye pointi 40.
Kati ya michezo 8 iliyosalia kwa Azam FC michezo mitatu atakuwa katika uwanja wake wa Azam complex, miwili katika uwanja wa Taifa, michezo minmgine katika uwanja wa Sokoine, Mabatini na Mkwakwani.
Azam FC michezo aliyobakisha:
15/03/14
AZAM FC Vs COASTAL UNION, U/azam
19/03/14
YANGA Vs AZAM FC, U/Taifa
26/03/14
AZAM FC Vs SIMBA SC, U/Taifa
02/04/14
RUVU SHOOTINGS Vs AZAM FC, Mabatini
06/04/14
MGAMBO JKT Vs AZAM FC, Mkwakwani
09/04/14
AZAM FC Vs JKT OLJORO, U/Azam
23/04/14
MBEYA CITY Vs AZAM FC, Sokoine
27/04/14
JKT RUVU Vs AZAM FC, U/Azam
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment