Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex uliopo Chamanzi, Azam FC waliandika goli la kwanza kupitia kwa Kipre Herman Tcheche akiunga pasi ya ndgu yake Kipre Bolue.
Kuingi kwa goli hilo liliwapoteza Coastal union na kuwafanya Azam FC watawale kwa kiasi mkubwa mchezo huo wa leo.
Katika dakika ya 38 Kipre Hermani Tcheche aliandikia Azam FC goli la pili baada ya kuunganisha krosi ya chipukizi Gardiel Michael na kuipeleka Azam FC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Azam FC wakionekana wakiwa na hamu ya kuandika goli la Tatu na huk Coastal union wakiwa wanasaka goli la kufutia machozi.
John Bocco 'Adebayor' aliiandikia Azam FC goli la 3 katika dakika ya 64 akipokea pasi toka kwa kipre Herman Tcheche, goli lililo wavuruga zaidi Coastal union na kuwafanya Azam FC kundelea kumiliki mpira.
Kelvin Friday aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Hamisi Mcha aliiandikia Azam FC goli la 4 akimalizia mpira wa Kipre Herman Tcheche katika dakika za lala salama.
Kwa matokeo hayo ya goli 4 - 0 Azam Fc wamefikisha pointi 43 baada ya kcheza micezo 19 bila kupoteza mchezo wowote ule.
Azam FC jumatano ya marchi 19 watawakaribisha Yanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment