
Waandaji hao wa michuano hiyo mifupi walipata goli hilo pekee katika dakika ya 64 kupitia kwa beki wa Azam fc Pascal Wawa aliyejifunga katika harakati ya kuzuia mpira wa faulo.
TP Mazembe walijaribu kutengeneza nafasi kadhaa ambazo zilikuwa zinaishia mikononi kwa Aishi Manula na mabeki wa azam fc kuondoa hatari hizo.
Azam fc nao hawakuwa nyuma katika kutengeneza nafasi ambapo waliishia kupaisha ama kipa wa TP Mazembe akiokoa hatari hizo na mchezo kumalizika kwa TP Mazembe kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Katika mchezo wa awali ulishuhudia ZESCO United ya Zambia waliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Don Bosco.
0 Maoni:
Post a Comment