Uongozi wa Azam FC umekanusha shutuma ya kusajili kiungo mwenye utata wa mkataba na klabu yake ya Simba SC, Ramadhani Singano "Messi".
Shutuma za Singano kusajiliwa na Azam FC zilikuja juu baada ya kusadikika kuwa Singano alionekana katika ofisi za Azam FC siku za karibuni.
Akizungumza na kituo kimoaja wapo cha redio, naibu katibu mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa "Father" amesema klabu ya azam fc haijafanya mazungumzo yoyote yale na Singano na wala hajamuona katika maeneo ya ofisi ya Azam FC.
"Ramadhan Singano sina hakika nalo kwasababu mimi sikumuona kwa macho yangu, hata kama kuna mtu alimuona sio tatizo, ofsi zetu si jela au mahakama, Singano ni mtu huru,anaweza kuonekana si tatizo", amesema Idrissa.
"Hakuna kandarasi yoyote tuliyoingia na Messi, hatujazungumza naye, narudia maneno yangu, kwa macho yangu sikumuona katika ofsi zetu" alisitiza Idrissa.
Ramadhani Singano 'Messi' anadaiwa na klabu yake ya simba sc kusaini mkataba wa mika mitatu, wakati yeye anadai kuwa alisaini mikataba wamiaka miwili ambao unaisha julai mosi mwaka huu, wakati mkataba unao tambuliwa na klabu yake unakwisha julai mwakani.
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment