
Katika mchezo huo Azam FC walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3-0, huku Adama City FC wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja.
Azam FC ambayo leo waliwapumzisha John Bocco, Frank Domayo na Salum Aboubakari na Aishi Manula walitawala mchezo kwa dakika zote 90.
Azam FC walianza kuona nyavu za wapinzani wao katika dakika ya 7 kupitia kwa Kipre Tcheche kabla ya kurejea tena nyavuni katika dakika ya 19.

Azam FC walipata goli la 3 kupitia kwa Faridi Mussa Maliki akimalizia kazi nzuri ya Amme Ally Zungu na kuipeleka Azam FC wakiwa mbele kwa goli 3-0.
Katika kipndi cha pili Azam FC walianza kwa mabadiliko ya kumpumzisha Pascal Wawa na nafasi yake kuchukuliwa na Said Morad.
Katika dakika ya 47 Mudathir Yahya aliiandikia Azam Fc goli la 4 na goli la 5 likifungwa na Aggrey Morice kwa mkwaju wa penati.
Azam FC wanamaliza hatua ya makundi wakiwa kinara wa kundi C, na huenda katika hatua ya robo fainali wanataraji kukutana kati ya Yanga na Khartoum Nation.
Azam FC leo: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Farid Mussa, Aggrey Morice/Gadiel Michael, Pascal Wawa/Said Morad, Abdallah Kheri, Mugereza Migi, Himid Mao, Mudathir Yahya, Kipre Tcheche/Didier Kavumbagu, Amme Ally
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment