Msemaji wa Azam FC Japhari Iddi Maganga amesem kuwa wachezaji wote wa Azam FC wamepewa mapumziko mpaka siku ya ijumaa, ambayo watarejea Chamanzi kwa ajili ya maandalizi na mchezo dhidi ya Yanga, agosti 22 mwaka huu.
Japhari Iddi Maganga amesema kuwa baada ya kurejea wachezaji watafanya mazoezi siku mbili kabla ya jumapili kuelekea Zanzibar kuweka kambi ya wiki mbili ya maandalizi ya mchezo huo wa ngao ya jamii.
Azam FC na Yanga wanataraji kukutana katika mchezo wa ngao ya jamii unao ashiria kuanza msimu mpya wa ligi kuu ya vodacom agust 22 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakati Azam FC wakitaraji kwenda Zanzibar, wapinzani wao teyari wapo Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
a
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment