Wednesday, November 23, 2011

Azam kucheza na Simba katika fainali ya uhai cup

Posted By: kj - 7:28 PM

Share

& Comment


Ilikuwa siku njema kwa Saimon Happygod Msuva katika siku ya leo baada ya kufanikisha ushindi wa Azam Academy leo katika uwanja wa Karume.

Msuva amechungulia nyavu mara tatu katika ushindi wa goli 3-0 walio upata vijana hao dhidi ya wenzao walio itwa kwenye kikosi cha taifa cha vijana Serengeti boys katika mchezo wa nusu fainali ya Uhai Cup.

Kwa ushindi huo Azam Academy watawakabili Simba SC katika mchezo wa fainali utakao chezwa katika uwanja wa Karume, ikiwa ni ukumbusho wamchezo uliochezwa jijini Arusha wa nusu fainali ya Rolling stone mwishoni mwa julai mwaka huu.

Katika mchezo huo mabingwa mara mbili Azam Academy waliichapa Simba B goli moja bila.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.