Monday, November 21, 2011

Azam kuwakabili Serengeti katika nusu fainali ya Uhai

Posted By: kj - 8:30 PM

Share

& Comment

Wakiwa bila ya nyota wake wa tano wanaocheza katika kikosi cha Serengeti Boys, Azam Academy wakiwatumia wachezaji chini ya miaka 17 wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya Uhai Cup inayo husisha vikosi vya vilabu vya ligi kuu chini ya miaka 20, baada ya kuisambaratisha Moro United.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Azam, uliamuriwa kwa mikwaju ya penati ambapo Azam Academy waliibuka kidedea kwa mikwaju 4-1.


Azam Academy ambayo ndio timu ilio chukua mara nyingi kombe hilo ambapo wamechukua mara mbili mfululizo kabla ya Ruvu Shooting walio vuliwa na Azam Academy, kunyakuwa kombe hilo msimu uliopita, watawafaa Serengeti Boys (timu ya Taifa chini ya miaka 17) katika mchezo wa nusu fainali utakao chezwa November 23.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utakao chezwa siku hiyo ni timu iliyofungwa na Azam Academy katika michuano ya Rolling stone katikati ya Mwaka huu Simba SC itawavaa wa Toto wa Yanga, Toto Africa ya Mwanza.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.