Saturday, November 12, 2011

Mwaikimba kuongeza kasi ya Azam katika kufumania nyavu

Posted By: kj - 3:42 PM

Share

& Comment

Mshambuliaji aliyezaliwa upya katika miwa ya Kagera, Gaudence Mwaikimba amemwaga wino wa kuitumikia Azam FC.

Mwaikimba ambaye alisajiliwa na Moro united mwanzoni mwa msimu huu na kuweza kufumania nyavu mara 6 akiwa nyuma kwa goli 2 za Mshambuliaji wa Azam FC John Bocco, huku akitoka kwenye ufungaji bora wa Kili Taifa Cup 2011, na akiwa nyuma ya Mrisho Khalfan Ngassa katika ufumania nyavu msimu uliopita akiwa Kagera Sugar.

Mwaikimba anachukuwa nafasi ya Mghana Abdul Wahab aliyeshindwa kutamba na uzi wa Azam FC, huku beki aliyetamba na Simba toka Uganda Owino akichukuwa nafasi Mghana Nafiu.

Kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo wa Zamani wa Yanga na Ashanti kunaimarisha safu ya ushambuliaji ya Azam inayoongozwa na John Boko, ambayo msimu huu imekuwa aitikisi nyavu kama ilivyo zoeleka katika misimu iliyopita.


Katika hatua nyingine Azam Academy imeanza vyema michuano ya Uhai Cup baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 pale walipo cheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Azam.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.