Friday, November 11, 2011

Tukawape sapoti vijana wetu

Posted By: kj - 5:50 PM

Share

& Comment

Pazia la Uhai Cup 2011 litafunguliwa hapo kesho katika viwanja viwili vya Azam na Karume jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Azam Academy kitafungua michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 20 kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu, kwa kuwavaa Kagera Sugar kesho saa 3 asubuhi katika uwanja wa Azam.

Azam Academy itashiriki michuano hiyo bila ya baadhi ya nyota wake walioitwa kwenye timu ya taifa chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' ambao nao watashiriki michuano hiyo.

"Uhai Cup 2011 inaanza Kesho saa 3 asubuhi, Azam Academy vs Kagera Sugar. Azam imejiandaa vizuri japo inakabiliwa na upungufu wa wachezaji walioitwa timu ya taifa ya U17,,,,mechi itachezwa Uwanja wa Azam na mechi nyingine Karume." toka kwenye page ya Azam FC katika Facebook.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.