Thursday, January 19, 2012
Azam kujipima kwa Fuon kabla ya kuanza ligi
Posted By: kj - 10:21 PMMabingwa wa Mapinduzi Cup –Azam FC hapo kesho jioni majira ya saa 10:30 itashuka katika uwanja wa Chamazi kukwaana na timu ya Fuoni FC ya Zanzibar.
Fuoni wanashiriki ligi kuu ya Zanzibar. Kiingilio katika mchezo wa kesho kitakuwa shilingi 2000 kwa jukwaa kuu na Shilingi 1,000 mzunguko.
Keshokutwa asubuhi majira ya saa 03:00 Fuoni watashuka tena dimbani kukwaana na Azam Academy. Mechi ya keshokutwa asubuhi haitakuwa na kiingilio.
Mchezo kati ya Azam FC na Fuoni ni wa tisa mfululizo kwa Azam FC huku ikiwa imeshinda michezo saba na kutoka sare mmoja.
Mchezo wa kesho ni wa mwisho wa kirafiki kwa Azam FC tangia ianze mazoezi kwa ajili ya raundi ya pili.
Azam FC ilicheza na JKT Ruvu na kuifunga 3-0 kabla ya kuifunga Yanga 2-0 na baadaye kwenda Zanzibar kushiriki mashindano ya mapinduzi Cup.
Ikiwa Zanzibar Azam FC iliifunga Kikwajuni 3-1, baadaye ikatoka sare ya 1-1 na Mafunzo kabla ya kuifunga Yanga 3-0 na Simba 2-0 na baadaye kuifunga Jamhuri 3-1.
Juzi Jumanne Azam FC iliifunga Villa Squad 3-2 na kesho itakwaana na Fuoni FC ya Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment