Kalunde Jamal
KOCHA mkuu wa Azam, Stewart Hall amesema ameiandaa timu yake kwa ajili ya kucheza na timu yoyote bila kujali ina uwezo gani.Hall alisema kudharau mechi kuna madhara makuu mawili kwanza kupoteza imani kwa mashabiki, lakini inaweza kuwaweka kwenye nafasi ya kushindwa kufikai malengo yake.
"Sifanyi maandalizi kwa ajili ya Simba au Yanga tunataka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu hivyo mechi zote za mbele yetu ni muhimu," alisema Hall na kuongeza.
"Kesho tutakuwa uwanjani tukiwakabili Afrikan Lyon tukishinda hapo utakuwa mwanzo mzuri kufikia malengo yetu."
Hall amesema hayo huku akiwa na kumbukumbu ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Lyon.
Azam ipo nafasi ya tatu na pointi 22 wakati Lyon yenye ipo nafasi ya nane na pointi 14 kabla ya mchezo baina yao utaochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi.
0 Maoni:
Post a Comment