Monday, January 2, 2012

Azam waanza kwa ushindi Mapinduzi

Posted By: kj - 8:08 PM

Share

& Comment


Wazee wa gonga Azam FC wameanza vyema michuano ya Mapinduzi Cup kwa kuichapa goli 3-1 timu toka Zanzibar Kikwajuni FC, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amana Zanzibar.

Azam FC wanatumia michuano hiyo kwa ajili ya kujianda na mzinguko wa pili wa ligi kuu, walifungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 13 kabla ya kumtengeneze John Boko goli la pili na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa Azam FC kuwambele kwa magoli 2-0.

Kijana toka visiwani Zanzibar Khamis Mcha Viali alihitimisha kurasa za magoli kwa kuiandikia Azam FC goli la 3 katika dakika ya 75, kabla ya Kikwajuni kujipatia goli la kufutia machozi kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa ufundi mkubwa ka ika dakika ya ya 82.

Kwa matokeo hayo Azam wanakwea katika usukani wa kundi B ambalo lina timu za Yanga na Mafunzo ambao wanacheza usiku huu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.