AZAM waliwasili jijini Dar es Salaam jana Ijumaa jioni kwa Boti ya Kilimanjaro wakiwa na kombe lao walilotwaa kwenye michuano ya Mapinduzi mjini Zanzibar na kuongezewa kitita kingine cha Sh10 mililioni na uongozi.
Timu hiyo tajiri iliyoweka rekodi ya kuzichapa mfululizo Simba na Yanga kwenye michuano hiyo, ilitwaa kombe baada ya kuifunga Jamhuri mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi usiku.
Ingawa viongozi wa Azam walikuwa wakifanya siri kubwa kwa madai kuwa si kitu cha ajabu wala cha kuandikwa gazetini, wachezaji wamedokezwa kuwa wamezawadiwa Sh10 milioni wagawane kama zawadi ya uongozi.
Hilo ni kombe la kwanza la Azam ya wakubwa kutwaa tangu iwe chini ya kocha Muingereza Sterwart Hall.
Mwanaspoti
Saturday, January 14, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment