Monday, January 16, 2012

Mwaikimba kupika magoli

Posted By: kj - 11:53 AM

Share

& Comment


Doris Maliyaga

MAKOCHA wengi Tanzania kilio chao kikubwa huwa ni kushindwa kufunga mabao kwa washambuliaji, hali ambayo mara nyingi huwasababishia matokeo mabaya kwa timu zao.

Kwani kati ya washambuliaji wote walio na sifa za kuwatoka mabeki na kuziona nyavu mara nyingi ni wachache Tanzania hii na siku zote majina yao hayabadiliki. Kama utawataja kwa majina, nyota mpya wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba kamwe huwezi kukosa kwani mara nyingi amekuwa akimpa raha kila kocha aliyefanya kazi naye na ataungana na John Boko 'Adebayor' (Azam) na Jerry Tegete (Yanga) kwa wazawa.

Jackson Mayanja, kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Uganda na kocha wa zamani wa Kagera Sugar, Hassan Banyai wa Moro United na Stewart Hall wa Azam hao ni miongoni mwa waliofanya kazi na Mwaikimba, hata siku moja, haijawahi kutokea walalamike juu ya nyota huyo huku wakimmwagia sifa kibao.

Alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Taifa 2011 akiwa na timu ya Mkoa wa Mbeya, lakini pia, huwa hakosi katika wakali wanaokuwa, wakiwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara. Kutokana na uhodari wake, Spoti Mikiki lilizungumza naye na yeye akaeleza malengo, pamoja na siri kubwa ya mafanikio yake.

''Naweza kusema, kufunga ni kazi yangu na naweza kufunga, ili mradi nipate nafasi ya kufanya hivyo,'' anasema Mwaikimba ambaye anaishabikia klabu ya Arsenal ya England.

''Nilifanya hivyo na Kagera Sugar, Moro United na sasa Azam FC
nitafanya hivyo na pengine zaidi ya hapo, kwa sababu nitakuwa nikicheza na wachezaji wenye buwezo na kulisha vizuri mshambuliaji,'' anaeleza Mwaikimba anayevutiwa na soka la Msweden, Zlatan Ibrahimovic nyota wa Barcelona aliyepelekwa kwa mkopo AC Milan.

Mwaikimba aliongeza na kueleza mazingira ya klabu yake mpya na kusema; ''Nafurahia mazingira ya Azam FC, kwani katika klabu zote nilizopita hii ni babu kubwa na naamini itanitoa.Tunaishi vizuri kwa ushirikiano, lakini pia hata mazingira ya kazi na programu za mazoezi na mechi, ziko vizuri, kiujumla nina furaha kuichezea Azam FC,'' anaeleza.

Kuhusu Taifa Stars, Mwaikimba anasema kuwa, atakapopata nafasi atafanya vizuri, kwa sababu kiwango chake si kigeni na kila mdau wa soka ameuona uwezo wake katika mechi za ligi anazocheza.

Mwaikimba ambaye ni mwenyeji wa Mbeya, katika familia yao wamezaliwa nane, wakike wakiwa wanne na wakiume wanne, lakini sasa wamebaki watatu baada ya mmoja wao ufariki. Kipaji cha soka alikuwa nacho tangu utoto, lakini alikuwa na kupata umaarufu mkubwa akiwa na klabu ya Ashanti FC ya jijini Dar es Salaam mwaka 2005.

Kiwango jicho ndicho kilipelekea asajiliwe na Yanga 2007 aliyoichezea hadi 2009 alipoachwa na kocha wa zamani wa kikosi hicho, Mserbia Dusan Kondic na ndiye anamlaumu alisababisha kiwango chake kushuka.

Hata hivyo alikaa nje ya Uwanja kwa msimu na kuibukia Prisons ya Mbeya, huko alirudisha makali yake na kung'aa ndipo akaenda Kagera Sugar na baada ya mwaka alikwenda Moro United na sasa ametua Azam.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.