Friday, January 6, 2012

Kipre amwaga cheche kwa kambi ya waathirika

Posted By: kj - 11:22 PM

Share

& Comment


Cheche zilidondoshwa katika uwanja wa Amani usiku huu, na mdondoshaji alikuwa Kipre Tchetche ambapo walipeleka maangamizi kwa kambi ya wahanga wa Mafuriko wa Jangwani, Yanga.

Utazungumza nini kwa vijana wa kapeti la Mbande, katika suala la kusafisha timu pinzani, huku Kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' alipewa Jukumu la kuongoza nafasi ya kiungo akisaidiwa na Abdulhalim Homoud, Kipre Bolou na Abdi Kassim Babi, walipata goli la kuongoza katika dakika ya 2 kupitia kwa Mshambuliaji hatari wa Azam FC, John Raphael Bocco kwa mkwaju wa penati.

Azam ikiwa chini ya ulinzi wa Aggrey Morise, Said Morad, Erasto Nyoni na Waziri Salum walipata goli la pili kutoka kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 29.

Azam walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2 bila, huku wakitawala mchezo kama ilivyo ada yao, na kupelekea baadhi ya wachezaji wa Yanga kuonekana mzigo katika timu yao.

Kipindi cha pili waliendelea kutoa burudani ambayo inaenda sambamba na upatikanaji wa magoli, na katika dakika ya 60 Kipre Tchetche alitupia goli la 3 na kuipeleka Azam FC nusu fainali ya Mapinduzi Cup na kuwaacha Yanga wakitoka matupu.

Azam FC na Mafunzo wamefanikiwa kutinga nusu wakitokea kundi B, huku Yanga na Kikwajuni wakiaga michuano hiyo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.