Monday, January 9, 2012

Wazee wakuzomewa wapeleka maafa msimbazi

Posted By: kj - 10:49 PM

Share

& Comment


Wachezaji wanaongoza kwa kuzomewa pale wanapo vaa uzi wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Gaudence Mwaikimba na John Raphael Bocco leo wamepeleka maafa katika kambi ya Msimbazi baada ya kumtungua Juma Kaseja (Kipa wa Simba) mara moja kila mchezaji.

Simba wamechapwa goli 2 bila katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya mapinduzi cup 2012, na Azam kutinga fainali ya michuano hiyo itakayo fanyika siku ya mapinduzi january 12 mwaka huu katika uwanja wa Amani.

Kama alivyo wafanya Yanga John Bocco alifunga goli lake la kwanza leo katika dakika ya 10 katika mchezo uliokuwa na kasi na ushindani wa hali ya juu. Goli la Bocco lilidumu kipindi chote cha kwanza.

Mtokea bench Gaudence Mwaikimba akiingia dakika ya 85 akichukua nafasi ya Muivorycoast Kipre Tchetche aliandikia Azam FC goli la pili katika dakika 90 ya mchezo, na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam kumchapa Simba goli 2-0.

Azam FC anangoja mshindi wa kesho katika nusu fainali ya pili ambapo Mafunzo watakwaana na Jamhuri ya Pemba.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.