Saturday, January 12, 2013

AZAM FC KUWEKA RIKODI MBELE YA TUSKER LEO?

Posted By: kj - 7:31 AM

Share

& Comment

Mabingwa wa mapinduzi cup Azam fc leo usiku watakuwa na kibarua mbeke ya Tusker katika mchezo wa kuweka rikodi kombe la mapinduzi katika mchezo wa fainali unao tarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Amani Zanzibar.

Michuano ya 4 ya kombe la mapinduzi inatarajiwa kuhitimishwa leo, huku kila mwaka ukitoa bingwa mpya, hivyo basi endapo Azam fc wakifanikiwa kutwaa ubingwa leo kwa kuifunga Tusker itakuwa ndiyo timu ya kwanza kutwa ubingwa huo mara mbili mfululizo.

Mtibwa sugar ndio wa mwanzo kulinyanyua kombe hilo mwaka 2010, wakifuatiwa na Simba sc mwaka 2011 na Azam fc kulitwaa hapo mwaka jana.

Kwa mara ya kwanza michuano hiyo inashirikisha timu kutoka nnje ya mipaka ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, na timu hiyo ambayo ni Tusker ya kenya ikifanikiwa kutinga fainali bila ya kupoteza mchezo wowote ule kama ilivyo kwa azam fc.

Azam fc itawakosa wachezaji wake 6 kwa kuwa majeruhi na wakitumikia adhabu pamoja na wale walio enda Ethiopia na kikosi cha stars. Wachezaji hao ni Salum Abubakary, Aishi Manul waliopo kwenye kambi ya starr, Kipre Bolou na Jabir Aziyi wanatunikia adhabu, Kipre Tchetche, Abdulhalim Homoud, Waziri Salum na John Bocco majeruhi.

Mchezo huo wa fainali utarushwa moja kwa moja na star tv

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.