Thursday, January 10, 2013

AZAM FC WATINGA TENA FAINALI BAADA YA KUWACHAPA SIMBA

Posted By: azam fans - 9:10 AM

Share

& Comment

Goli la Joackins Akudo lilipelekea mchezo kuamuliwa kwa mikwaju wa penati baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare za goli 2-2 na azam fc kushinda kwa penati 5-4 na kutinga fainali kwa mara ya pili mbele ya simba sc.

Mabingwa wa mapinduzi Azam fc walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Humphrey Meno katika dakika za mwanzo wa mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki lukuki wa visiwani humo.

Katika mchezo huo uliochezwa jana usiku katika uwanja wa Amani katika kisiwa cha Unguja, uliingia dosari katika dakika ya 14 kufuatia kukatika umeme uwanjani hapo, na mpaka kipindi cha kwanza kinakwisha azam walikuwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili simba sc walilisakama lango la azam na katika dakika ya 75 jitihada za simba zilizaa matunda baada ya Rashidi Ismail kuipa simba goli la kusawazisha na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.

Katika dakika 30 za nyongeza simba sc waliandika goli la pili katika dakika ya 10 kupitia kwa Miraji Madenge, goli lililo wachanganya azam na kupelekea Jabir Azizi na Kipre Tchetche kuzawadiwa kadi nyekundu.

Wakati mashabiki wa simba wakiamini kuwa wametinga fainali na mwamuzi akijiandaa kumaliza mchezo, azam walifanikiwa kupata penati katika dakika hiyo ya mwisho iliyotiwa kimiani na Joackins Akudo na kupelekea mchezo kwenda katika mikwaju ya penati ambapo azam walishinda kwa mikwaju 5-4.

Nusu fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa leo ambapo miembeni watakuwa wanapambana na tusker ya kenya wakati mchezo wa fainali ukitarajiwa kuchfzwa january 12 siku ya mapinduzi ya Zanzibar.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.