Tuesday, January 29, 2013

AZAM KUWAKABILI TOTO KESHO BILA YA BOCCO

Posted By: azam fans - 9:58 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa mapinduzi cup Azam fc wanataraji kuteremka katika uwanja wake wa azam uliopo Chamanzi jijini Dar es salaam hapo kesho bila ya mfumania nyavu wao John Raphael Bocco pale watakapo wakabili Toto Africa.

Azam na Toto Africa wanateremka kucheza michezo yao ya pili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom, baada ya ayam kutoka katika ushindi wa goli 3-1 na toto wakitokea kwenye kichapo cha goli hizo hizo 3-1.

Azam fc watashuka uwanjani tena bila ya huduma ya washambuliaji John Bocco na Kipre Tchetche kama ilivyotokea katika mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera sugar.

Brian Umony anatarajiwa kuwaongoza wazanzibar Hamisi Mcha na Abdi Kassim, huku wachezaji wengine wote ukiondoa Bocco na Kipre Tchetche wako fiti kwa mchezo huo wa kesho january 30.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.