Saturday, January 26, 2013

UMONY AIONGOZA AZAM KUICHAPA KAGERA

Posted By: azam fans - 7:09 PM

Share

& Comment

Mshambuliaji toka Uganda anaekipiga azam fc Brian Umony leo jioni ametengeneza nafasi ya magoli mawili na kuwa mwiba kwa Kagera sugar katika ushindi wa goli 3-1 walioupata azam.

Katika mchezo huo wa kwanza wa duru la pili uliochezwa katika uwanja wa azam complex, kocha wa azam fc Stewart alishusha kikosi bila ya kuwa na washambuliaji asilia.

Azam fc waliandika goli la kwanza kupitia kwa Abdi Kasim Babi katika dakika ya 20 akimalizia kazi nzuri ya Mganda Brian Umony na dakika 11 mbele Umonyi aliwazidi ujanja mabeki wa kagera na ktmpasi Khamisi Mcha aliyeifungia azam goli la 2 na kuifanya iende mapumziko wakiongoza 2-0.

Alikuwa ni Khamisi Mcha aliyeipatia azam goli la 3 katika dakika ya 71 kabla ya Paul Ngalema kuipatia kagdra sugar goli la kufutia machozi katika dakika ya 81 na kupelekea mchezo kumalizika kwa azam kushinda 3-1.

Kwa matokeo hayo ya leo azam hmeendelea kujikita nafasi ya pili kwa kufikisha point 27 point 2 nyuma ya vinara yanga.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.