Wednesday, January 30, 2013

AZAM WATANDIKA 3 NYINGINE NA KUFIKISHA 30

Posted By: azam fans - 8:00 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa mapinduzi cup Azam fc leo wameendeleza ushindi wao wa goli 3-1 mbele ya Toto Afrika ya Mwanza katika mchezo wa pili wa duru la pili wa ligi kuu ya vodacom.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa azam complex na kushuhudiwa na kocha mkuu wa timu ya taifa 'Taifa stars', azam waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 9 kupitia kwa Kipre Michael Bolou.

Ilichukuwa dakika 11 kwa Brian Umony kuipatia goli la pili azam na kupelekea mchezo kwenda mapumziko azam wakiwa mbele kwa goli 2-0, huku wakitawala mchezo katika kipindi chote cha kwanza.

Katika kipindi cha pili Azam walikianza vyema kwa kuandika goli la 3 kupitia kwa Humphrey Meno katika dakika ya 46 baada ya kugongeana vyema na Brian Umony.

Alikuwa mtokea benchi Selemani Kibuta aliyeipatia goli la kufutia machozit kwa Toto Afrika ya Mwanza katika dakika ya 77 na kupelekea mchezo kumalizika kwa ushindi wa goli 3-1 kwa azam fc.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.