Bocco na Tchetche huenda wakaanza katika mchezo dhidi ya mtibwa sugar utakao chezwa katika uwanja wa Manungu complex uliopo Ttriani Morogoro february 9 kabla ya kurejea Dar es salaam katika uwanja wa Azam complex kuwakabili wa Sudani kusini (Al nasri) hapo february 16.
Azam fc iliyo katika nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom february 16 mwaka huu wataandika historia mpya ya kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano yanayoandaliwa na shirikisho la soka Africa 'CAF' pale watakapo wakaribisha wageni wengine katika mashindano hayo ya CAF Al-Nasri ya Sudani Kusini katika michuano ya kombe la shirikisho.
Urejeo wa Bocco na Tchetche inapelekea orodha ya wachezaji walio majeruhi ndani ya azam kuwa tupu, na hivyo kumuongezea upana kocha Stewart Hall wa uteuzi wa wachezaji katika mchezo uliombele yake.
Azam fc imecheza michezo miwhli ya ligi kuu bila ya washambuliaji hao wawili na kufanikiwa kushinda goli 3-1 katika kilamchezo, huku wachezaji waliopewa jukumu la kuziba pengo la wafumania nyavu hao wa azam fc walifanya vyema kazi yao na kuonyesha uchu wa magoli.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment