Sunday, January 6, 2013

TCHETCHE KUKAA NNJE WIKI MBILI

Posted By: azam fans - 10:19 AM

Share

& Comment

Mshambuliaji wa Azam fc raia wa Ivory coast Kipre Tchetche atakuwa nnje ya uwanja kwa mda wa wiki mbili kutokana na jeraha la kifundo al4lopata juzi katika mchezo dhidi ya coastal union.

Tchetche atarajiwi kurejea katika michuano ya mapinduzi cup inayoendelea katika uwanja wa Aman visiwani Zanzibar kutokana na jeraha alilolipata katika mchezo wa kwanza kwa azam katika michuano hiyo ambayo azam ndiye bingwa mtetezi.

Tchetche anaungana na Waziri Salum anae uguza kidole chake, Abdulhalm Homoud aliyeumia katika kambi ya zanzibar heroes ikijiandaa na michuano ya chalenjh jijini Kampala na John Bocco katika orodha ya wachezaji waliyo majeruhi.

Bocco kwa sasa yupo India kwa ajiki ya matibabu ya jeraha alilopata akiwa anatumikia timu ya taifa, Kilimanjaro stars.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.