Mbio hizo za ubingwa wa Tanzania bara zimechukua sura mpya baada ya Yanga kwenda kuweka kambi ya wiki tatu nchini Uturuki, wapinzani wao Simba sc wakaanza na michuano ya kombe la mapinduzi kabla ya kuweka kambi ya wiki mbili nchini Oman.
Wakati simba na yanga wakiwa nnje ya bara la Afrika timu inayojaribu kupenya katikati yao wao walianzia Kinshasa DR Congo kabla ya kutetea kombe lao la mapinduzi na kuelekea Kenya waliko kaa kwa takriban wiki moja. Huku Coastal union wanao tolea udenda uaingwa wa bara wao wakianza na mapinduzi cup na kumalizia kambi yao hapa hapa Bongo kama ilivyo kwa timu nyingine shiriki.
JE NINANI ALIYEKUWA NA KAMBI BOQA YA MAANDALIZI YA MZUNGUKO WA PILI? ni swali linalopelekea wadau kungoja kwa hamu huo mzunguko wa pili utakao anza leo.
RATIBA YA VPL WIKIEND HII.
26/01/13
SIMBA SC Vs AFRICAN LYON
Simba sc watakuwa wanaanza maisha mapya ya bila jina la Emanuel Okwi katika ligi kuu ya vodacom pale watakapo wakaribisha Africa lyon iliyo katika janga la kushuka daraja.
Simba ilianza vyema mzunguko wa kwanza na kujikita kileleni lakini kuelekea mwishoni mwa mzunguko huo walijikuta na matokeo mabovu na kujikuta wanamaliza mzunguko wakiwa nafasi ya 3 na wakiwa nyuma kwa point 6 toka kwa vinara.
Lyon wao walianza vibaya msimu kulikopelekea kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa nafasi ya pili tokea mwisho.
Simba sc iliyochini ya kocha mpya toka Ufaransa atakuwa na kibarua cha kuendeleza ushindi mbele ya Lyon watakapo kutana katika nyasi za Taifa.
AZAM FC Vs KAGERA SUGAR
Msimu huu azam walifanikiwa kuvunja mwiko wa kufungwa na kagera sugar katika uwanja wa Kaitaba, na kesho wanakutana katika uwanja wa azam uliopo Chamanzi, uwanja wenye rikodi nzuri kwa upande wa Azam fc.
MICHEZO MINGINE
Coastal Union Vs Mgambo JKT, Mkwakwani Tanga
Ruvu Shooting Vs JKT Ruvu, Mabatini Pwani
Mtibwa sugar Vs Polisi Moro, Manungu Morogoro
JKT Oljoro Vs Toto Africa, Sh. Amri Abeid Arusha
27/01/2013
YANGA Vs T. PRISONS
Srku ya jumapili yanga watawakaribisha Prisons katika uwanja wa Taifa huku kukiwa na kumbukumbu ya kutoka ruluhu na wanajela hao katika mchezo wa ufunguzi wa msgmu huu.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment