Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Azam complex uliopo Mbande jijini Dar es salaam, ikiwa ni siku 4 toka watoke kuwapa kichapo Al-Nasri Juba ya Sudan kusini katika michuano ya kombe la shirikisho na ikiwa siku 4 kabla ya kucheza na vinara yanga katika uwanja wa taifa.
Azam fc imeshuka uwanjani mara 16 wakikusanya point 33 zikiwafanya washike nafasi ya 2 nyuma kwa 3 kwa vinara yanga walioshuka uwanjani mara 16 wakikusanya point 36.
Mara zote azam na jkt ruvu wanapokutana mchezo huo ni wa mvutano na kuvutia kutokana na timu zote kucheza soka la aina moja ambalo nilakuweka mpira chini na kutawala ufundi mwingi.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment