Kesho azam fc itamenyana na jkt ruvu katika uwanja wa Azam complex uliopo Chamanzi katika muendelezo wa ligi kuu ya vodacom.
Kocha msaidizi wa Azam fc ameiambia Bin Zubeiry leo asubuhi kuwa kiungo Abdulhalim Homoud ameelekea visiwani Zanzibar kushiriki msiba huku akisema Umony anataraji kuanza mazoezi leo hivyo basi Umony na Homoud watakosa mchezo wa kesho lakini ni matumaini yao jumapili katika mchezo dhidi ya yanga watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.
Alisema pia Kipre Bolou ameanza mazoezi ya gyme na anauwezekano mdogo wakuwemo kikosini hapo kesho lakini katika mchezo dhidi ya yanga atakuwa wemo.
Bolou na Umony waliumia katika mchezo wa kombe la shirikisho la mpira wa miguu Africa (CAF) dhidi ya Al-Nasri uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na azam kushinda goli 3-1.
Beki wa kushoto Waziri Salum anataraji kurejea kesho baada ya kuwa nje ya uwanja toka december mwaka jana akiuguza jeraha lake na sasa yuko fiti kuendeleza gurudumu.
Katika chumba cha majeruhi kwa kikosi cha Azam fc amebakia Samih Hajji Nuhu ambaye atakuwa nnje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment