Yanga na azam fc katika mwaka uliopita wa 2012 walikutana mara 4 huku azam wakishinda michezo miwili na yanga kushinda miwili.
Mchezo wa mwanzo kukutana ulikuwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kombe la mapinduzi, ambapo azam waliwachapa yanga na yanga kutolewa katika mashindano hayo yaliyo malizika kwa azam kutwaa ubingwa.
Azam na yanga walikuja kukutana katika mcheyo wa raundi ya pili ya ligi kuu msimu wa 2011/12 ambapo azam waliwachapa yanga goli 3 katika mchezn ulitawaliwa na fujo kwa mwamuzi kupigwa.
Yanga walikuja kuifunga azam katika mchezo fainali ya kombe la Kagame goli 2-0 kabla ya kujakuifunga tena azam katika mchezo wa duru la kwanza ligi kuu ya vodacom msimu wa 2012/13.
Jumamorh hii (february 23) azam na yanga watakutana kwa mara ya kwanza katika mwaka huu, huku timu zote zikiwa hazijapoteza mchezo wowote wa ligi kuu huku yanga wakitoa sare moja na mtibwa sugar wakati azam wakishinda michezo yote.
Azam na yanga wote wanapoint 36 zinazowaweka katika uongnzi wa ligi wakitofautiana katika tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa hivyo kuwaweka yanga katika uongozi.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment