Friday, February 22, 2013

AZAM KWENDA KAMPALA BAADA YA KUCHEZA NA YANGA

Posted By: azam fans - 7:12 AM

Share

& Comment

Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la shirikisho la mpira Africa, azam fc wanataraji kwenda Kampala nchini Uganda kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Al-Nasri Juba utakao chezwa kati ya machi 2 na 3.

Azam fc wanataraji kwenda Kampala siku ya jamatatu ama jumanne mara baada ya kumaliza mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya vinara yanga wenye point sawa na azam fc.

"Mechi yetu na yanga itakuwa kipimo chetu cha mwisho kabla ya kwenda Uganda", alieleza kocha mkuu wa azam fc Stewart Hall.

Azam na Al-Nasri utakuwa mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho na utachezwa katika mji wa Juba Sudani kusini, baada ya wali kushuhudia azam wakiibuka na ushindi wa goli 3-1 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.


Wakati huo huo azam wametuma mashushu Juba Sudan kusini kuandaa mazingira ya timu itakapo fikia na kuangalia mbinu za wapinzani wao wanavyncheza wakiwa katika uwanja wa nyumbani.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.