Monday, March 4, 2013

AZAM FC KUCHEZA NA BARRACK YC II YA LIBERIA

Posted By: kj - 10:52 AM

Share

& Comment

Wawakilishi wa Liberia katika kombe la shirikisho Africa, Barrack YC II imefanikiwa kutinga katika hatua ya pili ya michuano hiyo inayoandaliwa na shirikisho la soka Africa CAF baada ya kuitoa Jehanson fc ya Sieralione kwa jumla ya goli 1-0.

Barrack YC II sasa itakutana na wawakilishi wa Tanzania waliosalia katika michuano inayoandaliwa na CAF, Azam fc katika hatua ya pili katika kombe la shirikisho Africa.

Katika hatua ya kwanza iliyohitimishwa jana Barrack YC II walianzia nyumbani ambapo waliibuka na ushindi wa goli 1-0 kabla ya jana kulazimisha sare ya bila kufungana nchini Sieralion walipokaribishwa na Jehanson fc.

Wakati azam fc walianzia jijini Dar es salaam ambapo walishinda goli 3-1 walipo wakaribisha El-Nasri Juba, magoli ya azam yakifungwa na Abdi Kassim na Kipre Tchetche aliyefunga magoli mawili.

Mchezo wa marejeano ulichezwa hapo jana Juba na kushuhudia wenyeji El-Nasri Juba wakilala goli 5-0 toka kwa azam fc magoli yakifungwa na Khamisi Mcha 'Viali' aliyefunga magoli 3, John Bocco na Salum Aboubakary 'Sure boy' kila mmoja akifunga goli moja.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.