Shirikisho la soka nchini wameitaka azam fc kutobweteka na kuridhika kwa ushindi huo mnono walioupata katika hatua ya awali na kufanikiwa kutinga hatua ya pili, badala yake iwechachu ya kufanya vyema..
"Hata hivyo ni vizuri kwa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo (azam fc) wakautazama ushindi huo kama changammnto kwao kuhakikisha wanajipanga vizuri zaidi kwa raundi inayofuatia." ilieleza taarifa ya TFF.
Azam fc ndie mwakilishi pekee aliyesalia katika michuano inayo andaliwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF, baada ya simba sc na jamhuri ya Pemba kutolewa kwa jumla katika michuano ya klabu bingwa Afrika.
Katika hatua ya pili azam fc wataanzia ugenini nchini Liberia kati ya machi 15,16 na 17 watakapo karibishwa na Barrack YC II, kabla ya kurejeana jijini Dar es salaam kati ya april 5,6 na 7.
Barrack YC II imetinga katika hatua hiyo baada ya kuitoa Jehonson fc ya Siera lione kwa jumala ya goli 1-0, ushindi ambao Barrack YC II waliupata katika uwanja wake wa nyumbani kabla ya kwenda suluhu (0-0) katika mji wa Freetown Sieralione.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
www.aboodmsuni21.blogspot.com
[+255 657 184 421]
0 Maoni:
Post a Comment