Saturday, March 2, 2013

AZAM WAONDOKO, UMONYI NDANI

Posted By: kj - 11:24 AM

Share

& Comment

Mabingwa wa kombe la mapinduzi azam fc wameondoka alfajiri ya leo kwenda Sudan kusini wakiwa teyari kwa mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho la soka Afrika, wakimjumuisha mshambuliaji hatari aliyewakosa yanga Brian Umonyi katika msafara huo wa wachezaji 20.

Azam fc jumapili ya machi 23 watakuwa wageni wa Al-Nasri ya Sudani kusini, ukiwa ni mchezo wa marejeano, baada ya ule wa awali uliochezwa katika uwanja wa taifa jhjini Dar es salaam kumalizika kwa azam kutoka na ushindi wa goli 3-2, huku Kipre Tchetcge akidumbukiza mpira kwenye nyavu mara mbili.

Azam fc katika mchezo huo wa kesho wanaitaji sare ya aina yoyote ile, ila kwa mujibu wa kocha msaidizi Kally Ongala amesema kuwa wamejianda kwenda kushinda japo kuwa wanaimani wapinzani wao (Al-nasri) hawatakubali kufungwa kirahisi.

Wachezaji 20 walio ondoka alfajiri ya leo ni makipa MWADINI ALLY na AISHI SALUM MANUEL.

Mabeki ni; JOACKINS ATUDO, LUCKSON KAKOLAKI, DAVID MWANTIKA, WAZIRI SALUM, HIMID MAO na MALIKA NDEULE.

Viungo ni; KIPRE BOLOU, JABIR AZIZI, IBRAHIM MWAIPOPO, SALUM ABOUBAKARY 'SURE BOY', HUMPHREY MIENO, ABDI KASSIM 'BABI' na KHAMIS MCHA 'VIALI'.

Washambuliaji ni; JOHN BOCCO 'ADBAYOR', KIPRE TCHETCHE, BRIAN UMONY, SEIF ABDALLAH na GAUDENCY MWAIKIMBA.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.