Thursday, February 28, 2013

AZAM KUONDOKA JUMAMOSI,

Posted By: kj - 9:25 AM

Share

& Comment

Wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la shirikisho Azam fc wanataraji kuondoka jumamosi asubuhi kuelekea Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wa marejeano.

Katibu mkuu wa Azam fc amesema kuwa msafara wa azam fc unao kwenda Sudani kusini siku ya jumamosi machi 2 kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho utakuwa na watu 27, ambapo wachezaji watakuwa 20 na viongozi 7.

Nassoro aliongeza kuwa mchezo huo wanataraji utakuwa mgumu kwao kwa kuwa wapinzani wao Al-nasri pamoja na wao wana nia ya kusongo mbele kwa hatua inayofuata.

Katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam azam fc walishinda kwa goli 3-1 hivyo kuhitaji sare yoyote katika mchezo huo utakaochezwa jumapili machi 3 ama wasiruhu kufungwa tofauti ya magoli zaidi ya 2 ili kusonga mbele.

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.