Azam fc wakimchezesha kwa mara ya kwanza kipa namba 3 wa Taifa stars aliyeibuliwa na azam academy Aishi Salum Manuel huku wakicheza bila ya mlinzi wa kimataifa Joackins Atudo waliandika goli la kuongoza katika dakika ya 5 kupitia kwa John Bocco.
Polisi moro waliamka baada ya goli hilo kuingia na kupeleka mashambukizi katika lango la Azam fc na kuzibitiwa vyema na safu ya ulinzi ya azam fc iliyokuwa chini ya David Mwantike na Lackson Kakolaki huku walinzi wa polisi nao wakifanya kazi njema ya kuwaficha John Bocco, Kipre Tchetche na Khamisi Mcha.
Saeu ya ulinzi ya polisi moro ilikuwa inaongozwa na beki wazamani wa yanga na mtibwa sugar Chacha Marwa na kupelekea mchezo kwenda mapumziko azam wakiwa mbele goli 1-0.
Kipindi cha pili polisi moro walikianza kwa kasi na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la azam, na kupelekea azam fc kushindwa kufanya kama wanavyofanya kwa kupata magoli katika dakika 15 za mwanzo wa kipindi cha pili.
Polisi moro walipata goli la kurawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Makil Rambos katika dakika ya 65 baada ya mchezajiwa azam kuushika mpira katika eneo la hatari.
Kocha msaidizi wa azam fc Kally Ongala aliyevaa kofia ya mkuu wake Sterwat Hall aliyekuwa jukwaani leo akitumikia adhabu yake, aliwapumzisha Jabir Azizi na John Bocco na kuwaingiza Michael Bolou na Abdi Kassim mabadiliko ya liyo shindwa kubadili matokeo na mchezo kwisha kwa sare ya 1-11
Azam fc leo, aishi salum, malika ndeule, waziri salum, david mwantika, lakson kakolaki, jabir azizi/bolou, humphrey mieno, salum aboubakary, khamis mcha/uhuru, john bocco/abdi na kipre tchetche
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 Maoni:
Post a Comment