Katika mchezo huo utakao chezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani, azam fc watashuka bila ya kocha wao Muingereza Stewart John Hall akiwa anatumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu.
Wachezaji wote wa azam fc wako teyari kwa mchezo huo ukimuondoa Samir Hajji Nuhu aliyemajeruhi,.
Azam fc ikiwa nyuma kwa point 6 toka kwa vinara wa ligi kuu, mchezo dhidi polisi moro iliyo katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 18 unaweza ukawa wa mwisho kwa azam kabla ya kwenda Liberia, ambapo wanataraji kuondoka jumatano ya machi 13 kwa ajili ya mchezo wa kwanza hatua ya pili katika kombe la shirikisho.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
NDIO SULUHISHO LA TATIZO YA COMPUTER YAKO
+255-657-148-283 (Habib)
+255-657-184-421 (Msuni)
www.aboodmsuni21.blogspot.com
0 Maoni:
Post a Comment