Ongala ameshatuwa nchini Moroco sambamba na msafara wa kwanza wa azam fc wenye jukumu ya kuweka mazingira yatakayo fikiwa na kikosi cha azam fc kinacho tarajiwa kuondoka kesho jumapili (aprili 28) saa kumi na moja jioni kuelekea nchini Moroco.
Afisa habari wa azam fc Japhari Iddi Maganga akizungumza na moja ya kituo cha redio kutokea Moroco amesema kuwa msafara wa kwanza wa Azam fc umeshatuwa salama nchini humo, wakiwa na kazi kubwa ya kuandaa mazingira timu itakapo fikia.
Katika msafara huo wa kwanza uliojazwa na viongozi wa azam fc akijumuishwa na kocha msaidizi Muingeleza Kally Ongala.
Maganga aliongeza kuwa msafara wa pili utaondoka kesho na kutuwa Moroco kesho kutwa siku ya jumatatu.
Naye kocha msaidizi Kally Ongala amesema kuwa hali ya hewa ya huko ni nzuri kutakona na kuwepo kwa baridi ambayo haiwachoshi wachezaji.
Azam na AS FAR Rabat wanatarajiwa kukutana tena siku ya jumamosi mei 4 mwaka huu katika mchezo wa marejeano, baada wa awali kumalizika kwa sare ya bili kufungana. Mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na star tv.
0 Maoni:
Post a Comment