Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa azam fc ndani ya facebook, inaeleza kuwa wamefika salama na wamepewa basi walilotumia kusafiria toka Casablanca mpaka Rabat.
"Azam FC imetua salama Casablanca na kusafiri kwa basi umbali wa kilometa 100 hadi Rabat na kufikia katika hoteli ya Golden Tulipo mjini
Rabat," ilieleza taarifa toka katika ukurasa wa azam fc.
Msemaji wa Azam fc Japhari Iddi Maganga akizungumza na moja ya redio hapa nchini, akiwa huko Moroco amesema kuwa wenyeji wao AS FAR Rabat waliwapokea vizuri katika uwanja wa ndege wa Casablanca na kuwapatia basi lililowafikisha katika mji wa Rabat.
Maganga aliongeza kuwa wachezaji leo watapewa mapumziko kutokana na uchofu wa safari ulichuku takribani masaa 15 na kesho wanataraji kuendelea na program ya maandalizi dhidi ya mchezo huo utakao chezwa jumamosi.
Msafara wa pili wa Azam fc uliondoka nchini jana mida ya jioni wakitumia ndege ya Emirates wakipitia Dubai ambapo walilala jana kabla ya kuunga safari ya kuelekea Casablanca, Moroco.
Azam fc wanaitaji sare ya magoli katika mchezo huo baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
0 Maoni:
Post a Comment